Tuesday, April 16, 2013
VITU KUMI AMBAVYO LABDA HUKUVIJUA au KUVIFIKIRIA
1. Kuna watu si chini ya watano katika Dunia hii wanakupenda sana, kiasi cha kuweza kufa kwa ajili yako na wengine zaidi kumi na tano wanakupenda kwa namna flani.
2. Kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu akuchukie ni kutokana na huyo mtu kutaka kuwa kama wewe.
3. Tabasamu lako lina uwezo wa kuleta furaha kwa mtu yeyote hata kama anakuchukia.
4. Usiku unapofika, na kabla hawajalala kuna watu ni lazma wakuwaze wewe.
5. Bila wewe, kuna mtu asingekuwa anaishi.
6. Fahamu kwamba kuna mtu au watu ambao hata huwamfahamu ila wanakupenda.
7. Unapokikosa kitu, fahamu kuna kitu kingine kizuri zaidi kinakuja toka kwenye hicho kitu.
8. Unapokuwa na fikra ya kutokuwa na nafasi ya kupata kile unachokitaka hakika hutokipata, ila kama unajiamini kama sio leo basi kesho utakipata.
9. Mara zote kumbuka sifa na pongezi unazopewa na achana na maneno yanayokatisha tamaa.
10. Jitahidi kuwaeleza watu vile unavyojisikia juu yao, hakika utajisikia raha zaidi pale watakapojua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment