German Shepherd Aina Ya Mbwa Aliyemtafuna Mmiliki Wake |
Polisi wamesema, sababu iliyopelekea mbwa huyo aina ya German Shepherd kumtafuna mmiliki huyo, ni kutokana na njaa aliyokuwa nayo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kula.
Polisi wakazidi kueleza, marehemu aliyekuwa na umri wa miaka 72 alifariki akiwa ndani ya nyumba ambayo alikuwa anaishi na mbwa huyo.
Wiki iliyopita majirani ilibidi watoe taarifa kwa maofisa wa Polisi wa Valencia baada kuhisi harufu kali iliyokuwa inatoka ndani ya nyumba hiyo.
Maofisa hao walipatwa na butwaa mara baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo na kukuta karibia nusu ya mwili wa marehemu ikiwa imetafunwa.
Mbwa huyo ambaye alikuwa akibwaka kwa muda mrefu, alikutwa akiwa na damu mdomoni mwake, na inaaminika mwanamke huyo alikuwa na maradhi yaliyopelekea kifo chake.
Hakika ni habari ya kusikitisha sana, je nini tunajifunza kutokana nahabari hii...?
No comments:
Post a Comment