Diamond Platnumz |
Msanii wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnum, amesema
atamuenzi Marehemu Bi Kidude kwa kuimba moja
kati ya nyimbo zake, Diamond amesisitiza kuwa wimbo atakaouimba utakuwa ni hit
singo ambayo hata na yeye akija kufa jamii itambue kwamba alifanya kitu kwa
ajili ya Bi Kidude.
Msanii huyo alizungumza hayo alipokuwa akiongea na mimi kupitia kipindi cha The Takeover cha TBC fm ambapo alisema “ntaimba nyimbo yake moja, ndio maana unaniona nipo nafanya research, kwa sababu nyimbo yenyewe ntakayoimba pia nataka niimbe na ibaki, hata mimi nikifa watu wanikumbuke kupitia nyimbo hiyo na ipendwe na watu pia.”
Katika hatua nyingine msanii huyo amewalaumu ma-producer wa
nyimbo yake ya Mapenzi Basi, hii imekuja baada ya nyimbo hiyo kuachiwa bila
ridhaa yake. Diamond amesema biashara ya kufanya kazi kiushikaji huwa inaponza
sana na dawa yake ni kuacha kufanya kazi kindugu.
“Nimejisikia vibaya kinoma yani, nimeona kama nahangaika
kufanya kazi halafu mtu kazi yangu anaichukulia masihala tu, lakini hiyo
inatokana na kufanya kazi kindugu na marafiki studio” aliongeza na kusema “kwa
sababu nyimbo kama ya Kesho hakuwahi kuvuja ilitoka ontime, lakini hizi kazi za
kindugu ndugu ndio hupelekea watu kuvujishiana nyimbo kijamaa, yani sio freshi”
alimaliza Diamond.
Wakati huo huo kutokana na kuvuja kwa nyimbo hiyo ya Mapenzi
Basi na kukubalika kwa wimbo wake wa Ukimuona ambao nao ulivuja mara baada ya
simu yake kuibiwa, Diamond ameruhusu rasmi kwa nyimbo hizo kuchezwa redioni.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, haitakuwa na maana
kuzizuia nyimbo zisichezwe redioni wakati tayari nyimbo hizo tayari watu wanazo kwenye simu
zao.
Amesisitiza kwa kusema “kama watu wakizichagua na kutaka zichezwe
basi ni ruhsa kufanya hivyo” alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment