Tuesday, April 16, 2013

KIPI KINAUMA ZAIDI KATI YA HIVI..?

1. Baada ya kufanya kazi mwezi mzima unafukuzwa kazi bila mshahara.
2. Ukiwa una download kitu kwenye mtandao inafika 99% alafu inagoma.
3. Unaingia na kibomu kwenye pepa halafu unabambwa.
4. Unanunua simu kwa bei kubwa leo hqlafu kesho zinawekwa kwenye promo zinauzwa bei nusu ya ile uliyonunua wewe.
5. Unamualika Demu mkali kwenye dinner unaagiza samaki alafu mwiba wa samaki unakukaba kooni.
6. Una muita demu wako geto kunaniii alafu anakuja na rafiki zake.
7. Unavunja uhusiano na girlfriend au boyfriend wako halafu siku inayofata unampata demu au jamaa mkali kuliko wewe.
8. Unanunua pafyumu kali lakini kwapa bado linatema.
9. Unafanya kazi kwenye kampuni miaka 10 bila kupandishwa cheo na kuongezewa mshahara.
10. Unamdanganya mkaba roba kuwa huna simu halafu inaita.
11. Unagombana na mtu barabarani hhalafu kufika ofisini unapokwenda kuomba kazi unamkuta anakufanyia interview.
12. Kama gari lako linatumia muda mwingi gereji kuliko barabarani.
13. Kwenye pepa matokeo yanatoka umefeli somo unaloliweza.
14. Unaingia kwenye pepa halafu unasahau jina lako la kwanza.
15. Unasajiliwa kama beki kwenye timu ya barani ulaya halafu jaribio la kwanza unapewa kumkaba Lionel Messi.
16. Kama mtoto wako wa pekee anajiunga na JWTZ kisha kupelekwa vitani.
17. Kama ukikosea ukaweka super glue machoni badala ya dawa ya macho.
18. Kama utapiga picha photoshop lakini bado unaonekana mbaya.
19. Kama panya atakula jina lako tu kwenye Cheti chako muhimu.

VIPO VINGI KILICHOBAKI KAZI NI KWAKO..!

No comments:

Post a Comment