Tuesday, April 16, 2013
KUWA PEKE YAKO SI UPWEKE
Ni bora niwe peke yangu kuliko kupoteza muda kwa mtu ambaye hatokuja kuwa na upendo wa dhati.
Ni bora nikae na kuangalia mahusiano ya wengine wenye furaha kuliko kwa mimi kujiingiza kwenye kitu kitachokuja kunifanya nijute.
Ni bora niwe mpweke kuliko kujiona niko peke yangu wakati mtu ninae.
Ni heri nisubiri atokee mtu ambaye toka moyoni mwake kweli atahitaji kuwa na mimi kuliko kumkimbilia mtu ambaye lengo lake ni kuuchezea moyo wangu.
Si kweli kwamba kuwa peke yako mara zote inamaanisha UPWEKE, ni kama vile unapokuwa kwenye mahusiano si kweli kwamba mara zote inamaanisha kuwa na FURAHA....!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment