Gabrielle Union |
Si kitu cha kushangaza kwamba Gabrielle Union alichaguliwa
kuwa mmoja kati ya wanawake wazuri kwa mwaka huu.
Ameungana na viwango
vya kina Halle Berry, Kelly Rowland na Kerry Washington kwenye toleo hilo
linalowahusu nyota wakali toka Hollywood.
Alipoulzwa amewezaje
kujiweka na kuonekana bado kijana na mrembo, alijibu:
"Nilianza kunywa
galoni la maji kwa siku nilipokuwa katikati ya miaka ya thelathini.
Yamebadilisha kila kitu kutoka kwenye kuujenga uzito, nywele, ngozi, kucha na
mfumo wa usagaji wa chakula. Na kwa kuongeza, naonekana kijana sababu natoka na
vijana. Naamini hiyo ndio sababu na inafanya kazi vizuri kwangu.
Amelieleza jarida
hilo kwamba katika umri wa miaka 40, ndio muda ambao siku zote alikuwa anataka
kuwa.
Kwa sasa Gabrielle
anatoka na nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani aitwae, Dwayne Wade, ambae
amemzidi miaka 9.
No comments:
Post a Comment