Mike Tyson |
Suarez ametozwa faini na klabu yaya Liverpool na anategemea
kupewa adhabu na chama soka cha Uingereza, adhabu inayoaminika kuwa itakuwa ni ya
kufungiwa kucheza mechi kadhaa kutokana na
kitendo hicho, tukio hilo lilitoke wakati timu hizo zilipokutana na kutoka sare
ya 2-2 kwenye uwanja wa Anfield.
Kitendo kama hicho
pia kiliwa kufanywa na Tyson kwenye pambano lake alilokuwa akipigana na Evander Holyfield
mnamo mwaka 1997. Kupitia kipindi cha Glenn David nchini Marekani Tyson alikuwa
na uhakika Suarez atamalizana na suala hilo.
“Nilimuona huyu jamaa kwenye Twitter na nikafikiria juu ya
hatma yake itakuwaje,” Tyson alisema,
kwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye
wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea na mtangazaji huyo Tyson alisema “Unajua kwamba jamaa alimng’ata
mtu, sote tunajua kwamba upumbavu hutokea popote, nadhani unafahamu nini namaanisha? Nina hakika atakuwa
ameomba msamaha kwa huyu jamaa. Niliomba msamaha kwa Evander na kila mmoja anaendelea na maisha yake.”
Suarez tayari ameshasema kwamba Ivanovic amekubali msamaha
wake kutokana na kitendo hicho, japo kuna mapendekezo kwamba hiyo inaweza kuwa sio
ishu ya msingi kuepekana na adhabu itakayomkabili.
No comments:
Post a Comment