Tuesday, April 16, 2013
DAWA YA MOTO NI MOTO
Mtu na mkewe wanagombana chumbani, ghafla ugomvi unakuwa mkubwa mke anaamua kukusanya vitu vyake kwa lengo la kuondoka.
Mume anashangaa anamuuliza, "Unakusanya vitu unaenda wapi?"
Mke kwa nyodo anajibu, "Nakwenda kwa mama yangu."
Mume naye akaanza kukusanya nguo zake na kuweka kwenye mabegi yake.
Mke kwa jeuri akamuuliza mume wake, "Unapaki unakwenda wapi?"
Mume akajibu kwa tabasamu, "na mimi nakwenda kwa mama yangu."
Mke akauliza tena "Hawa watoto wako watabaki na nani?"
Mume kwa kujiamini akajibu "nao waende kwa mama yao kama sisi tunavyokwenda kwa mama zetu."
Hiyo imesimamaje......!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment