Tuesday, April 16, 2013
AUZIWA BIKIRA YA KICHINA
Habari DC,
Mimi ni mume kwenye ndoa, na nataka nielezee ishu yangu na maumivu niliyoyapata pale nilipogundua kwamba, mke wangu ambae nilikuwa nafikiria ni bikira pale nilipomkuta sio bikira.
Mwanzoni kabla hatujaoana alinieleza kwamba yeye ni bikira, ila kitu cha kushangaza nimekuja kugundua kwamba kumbe alikuwa anafanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Hakika nilishtuka na kujisikia vibaya, nilimuuliza kama hii inamaanisha kwamba hakuwa bikira kabla hatujaoana, na akasisitiza kwamba alikuwa nayo.
Nilijiona mpumbavu na mjinga zaidi ya bwege, kwamba kwa nini niliuziwa mbuzi kwenye gunia.
Ni nini unadhani natakiwa kufanya? Kile nilichokuwa nakifikiria ni kweli kumbe hakikuwapo. Kiukweli najiona nimeangamia, nifanye nini jamani...?
Tunamsaidiaje huyu mdau japo kwa neno moja tu la matumaini...?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment