Tuesday, April 16, 2013
JOE BARTON ASEMA MAGRETH THACHER HASTAHILI PEPO
Mcheza kiungo wa The Olympique de Marseille ya ufaransa ameitwa na chama cha mpira wa miguu cha Ufaransa baada ya kumuita mlinzi wa timu ya Paris Saint-Germain Thiago Silva 'mvulana msichana bwanyenye' kupitia ukurasa wake wa twitter.
Olympique Marseilles wametoa tamko la kuomba radhi kwa niaba ya mchezaji huyo mtukutu, ‘Olympique Marseilles na Joey Barton wanaomba radhi kwa Thiago Silva na klabu yake kwa maneno mabaya yaliyosemwa na mchezaji wa muingereza ambayo aliyaaandika masaa 36 yaliyopita,’ taarifa hiyo ilisema.
Uongozi wa Olympique Marseilles umemtaka Joey Barton amalizane na mlinzi huyo toka Brazil. Nae Joe Barton ameahidi kumaliza tofauti zake na Thiago Silva.
Wakati huo huo, Joe Barton, amemuelezea wazili mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher, ambae alifariki juzi akiwa na miaka 87, kama ni ‘mzee mchawi’ ambaye hastahili kufika peponi’.
‘Naweza sema ‘pumzika kwa amani Maggie’, ila inaweza kuwa sio kweli kabisa. Kama pepo ipo, basi na kule hakutakuwa na nafasi ya huyu mzee mchawi’, Barton pia aliandika kwenye Twitter.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment