Monday, August 20, 2012

Msanii Keko Wa Uganda Amekuwa Chizi?Keko

Keko

Mitandao mingi ya kijamii imeejaa habari za rapa wa kike kutoka Uganda zikisema kwa amekuwa chizi, na hiini baada ya kuonekana akimkimbiza kibaka wa laptop.
Mitandao hiyo ya kijamii pia imeeleza kwamba Star huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter jinsi gani Uganda imekuwa si sehemu salama kwake na kuna watu wanahatarisha maisha yake, watu ambao walitaka kufahamu zaidi kuhusu stori hiyo, walijaribu kumpigia simu lakini matokeo yake ilipokelewa na dereva wa boda boda na hata alichokiongea kilionekana kutokuleta maaa yoyote.
Kitendo hicho cha Keko, kimewalazimu baadhi ya watu kuhitimisha kuwa amechizika, habari za hivi karibuni zinadai kuwa uchizi wa stori ya Keko ulikuwa ni stunt tu, aliyoitumia kufanya utafiti kujua ni kiasi gani anajulikana na watu
Keko ambae sasa yuko chini ya Sony Music Entertainment ameahirisha uzinduzi wa album yake mara tatu sasa ambapo alitangaza kuizindua mwezi wa nne tarehe 17 mpaka mwezi wa tano tarehe 4 na sasa kuipeleka mpaka mwezi wa nane tarehe 10, na inasemekana Sony nao wanataraji kutangaza siku yao ya kuzindua album hiyo.

No comments:

Post a Comment