Monday, August 20, 2012

Goldie Wa Big Brother Kuja Bongo

Prezzo & Goldie
Goldie ambae alikua mwakilishi wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa 2012 amethibitisha kwamba anakuja Tanzania mwanzoni mwa September 2012 kwa ajili ya kazi moja tu.
Goldie anakuja kwa ajili ya kutimiza lengo lake la kuingia studio na kurekodi kolabo na Ambene Yesaya a.k.a AY tu.
Amesema anafurahi kujua anakuja Tanzania ambapo tayari Ay ameshamuahidi kumpeleka na kumuonyesha sehemu mbalimbali za Tanzania.
AY
Goldie ambae ali-fall inlove kwa Prezzo wa Kenya alimfahamu Ay kwa Prezzo ambae alikua anamuongelea sana, pia kupitia nyimbo zake zilizokua zikipigwa kwenye jumba la Big Brother na hasa wakati alipokua akigombana na Prezzo.. Big Brother alikua anapiga single ya Ay na Sauti Sol wa Kenya ya I dont wanna walk alone.

No comments:

Post a Comment