Monday, August 20, 2012

Man to Watch

Mbwana Samatta
Ilikuwa ni dakika ya 44 krosi toka kwa Trésor Mputu inatua kichwani kwa MBWANA SAMATTA na kuandika bao la pili, full time Zamalek 1 v TP Mazembe 2
Nyota wa Tanzania, Mbwana Ally Samata, jana alipiga Bao la pili na la ushindi kwa Timu yake TP Mazembe iliyoifunga Al Zamalek bao 2-1 katika Mechi ya klabu bingwa barani Afrika iliyochezwa huko Cairo, Misri bila ya Watazamaji wowote kufuatia kuzuiwa kwao kuingia kwenye Mechi baada ya Vifo Uwanjani kutokana vurugu mapema Mwaka huu.
TP Mazembe ya Congo DR ilitangulia kupata bao katika Dakika ya 34 lililofungwa na Hichani Homoonde na Al Zamalek wakasawazisha Dakika moja baadae kwa bao la Razak Omotoyossi.
Al Ahly ya Misri walitoka sare bao 1-1 huko Ghana na Bechem Chelsea lakini bado wanaongoza Kundi B wakiwa na Pointi 10 wakifuatiwa na TP Mazembe.
Katika michuano ya kombe la shirikisho, timu iliyoitoa Simba ya Tanzania  Al Ahli Shandi kutoka Sudan ilipata ushindi ugenini wa bao 1 – 0 dhidi ya GD Interclube ya Angola.
 

No comments:

Post a Comment