Sunday, December 11, 2011

Kisaka kuja na Video Production

Producer Kisaka ndani ya Emotion Record
Producer anayekuja kwa kasi katika mziki wa Bongo fleva nchini Kisaka Michael kutoka Emotion Records, ni producer aliyejulikana baada ya kutengeneza albam ya Sam wa Ukweli ambayo inafanya vizuri sokoni, pamoja na albam ya Dullayo, hapo ndipo watu wakaanza kumfahamu Kisaka katika tasnia ya mziki huu wa kizazi kipya.
Akizungumza nami Kisaka alisema kwa sasa anatarajia kufungua kampuni ya video production.
Kisaka alizaliwa june 2 mwaka 1984 yombo jijini Dar es salaam, alimaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi yombo mwaka 1999.
Kipindi yupo darasa la sita alikua anapenda sana mziki hasa alipokua kanisani alipenda sana kujifundisha kupiga kinanda, na ndipo baadae akawa mpiga kinanda wa kanisa, na hapo ndipo alitamani siku moja aje kuwa producer.
Katika maisha yake ndoto yake kubwa ilikuwa aje kuwa Doctor lakini mpango sio matumizi wala haikua hivyo na akajiona anaangukia kwenye utayarishaji wa muziki.
Baada ya kufika kidato cha nne ndipo alianza kujifundisha kuwa producer, katika studio za Mawingu Records Msasani Dar es salaam.
Katika maisha yake producer aliokuwa anawakubali ni P. Funky Majani kutoka Bongo Records na marehemu Roy.

No comments:

Post a Comment