Wednesday, April 16, 2014

Kutana na Mchezaji Mwenye Miaka 18, Mlinzi wa Chelsea Anayelipwa £20,000 kwa Wiki Ambaye Hajawahi Kucheza Kwenye Kikosi cha Kwanza cha Timu.. na Pia Hategemei Kucheza kwa Siku za Karibuni

Ndani ya Emirates hapo kesho Alhamisi jioni, mchezaji anayelipwa hela nyingi kwenye historia ya Kombe la FA kwa vijana anategemea kucheza kwenye timu yake ya Chelsea katika mchezo wa pili wa nusu fainali dhidi ya Arsenal.

Anaitwa Andreas Christensen, ambaye  hakuna mtu aliyewahi kumuona uwanjani, ametimiza umri wa miaka 18 mnamo April 10. Analipwa £20,000 kwa wiki huku akiwa hajawahi kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu yake ya Chelsea.

Kuna kitu, sehemu fulani, naamini hakiko sawa pale ambapo mchezaji wa kikosi cha timu ya vijana analipwa kiasi hicho cha hela.





No comments:

Post a Comment