Wednesday, December 25, 2013
Pope Francis Ahutubia Kwenye Ibada Yake ya Kwanza ya Mkesha Wa Krismas Akiwa Pope wa Kanisa Katoliki [PICHA]
Pope Francis alifanya Ibada yake ya kwanza ya mkesha wa Krismasi akiwa kama Pope usiku wa Jumanne ndani ya St. Peter's Basilica, Vatican.
Kwenye Ibada hiyo ya kwanza akiwa kama Pope wa Kanisa Katoliki, Pope Francis aliwataka watu kuacha majisifu na ubinafsi na kufungua mioyo yao kwa Mungu.
Francis, ambaye amekuwa mtu wa kwanza kushika wadhifa huo toka nje ya Bara la Ulaya ndani ya miaka 1,300 mnamo mwezi March baada ya kujiuzuru kwa Pope Benedict IX, alihutubia maelfu ya watu waliojazana St Peters Basilica ndani ya Jiji la Vatican kwenye Mkesha huo wa Krismas.
Kwenye Ibada hiyo ya Mkesha wa Krismas Pope aliwataka Waumini kuwa na moyo wa kuwapokea wenzao kwa mioyo iliyo wazi.
Labels:
NEWS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment