Wednesday, December 25, 2013

Bomu la Kwenye Gari Lalipuka na Kuuwa Watu 14 Nje ya Kanisa Nchini Iraqi

Wakristu wa Iraqi Wakishiriki Kwenye Mkesha wa Krismas
Ndani ya Kanisa la St. Joseph Chaldean la Baghdad [Reuters]
Maafisa nchini Iraqi wamesema kumetokea mlipuko nje ya Kanisa moja Kusini mwa jiji la Baghdadna kuuwa watu kama 14 hivi.

Mlipuko huo umetokea leo Jumatano, karibu na Doha, ambapo Waumini walikuwa wanasali kwenye Ibada ya Krismasi, siku ambayo Wakristu wanaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu.


Mlipuko huo pia umejeruhi watu 30, na inaelezwa kuwa ni bomu lililokuwa kwenye maegesho ya magari na lililipuka wakati watu wakiwa wanatoka Kanisani baada ya kumaliza maombi, chanzo cha Polisi kimesema.

Wengi waliathiriwa na tukio hilo walikuwa ni Wakristu, chanzo hicho kiliongeza.

Mpaka sasa hakuna aliyetajwa kuhusika na shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment