Friday, December 20, 2013

Mawaziri Wang’atuka Sakata la Tokomeza Ujangili


KWA UFUPI

Mawaziri waliopoteza ajira zao usiku huu ni
Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), 
David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), 
Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani)
na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili.

Mawaziri waliopoteza ajira zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

Akizungumza Bungeni Dodoma usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.

“Tulifanya operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda. “Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”

Katika mdahalo uliogusa nyoyo za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.

Chanzo: Gazeti MWANANCHI

No comments:

Post a Comment