Friday, December 20, 2013

Kutoka Bungeni: Waziri wa Maliasili Mh. Hamis Kagasheki Atangaza Kujiuzulu Uwaziri


Waziri wa Maliasiri na utalii atangaza kujiuzuru rasmi akiwa ndani ya bunge.

Asema yeye ni mtu mzima na kasikia mengi, kateuliwa na rais kwa matakwa ya rais na hakuomba hivyo ana resign.

Mathayo yeye anadai ameshutumiwa mambo mengi kama sena na mgumo vyote vipo ila hakuhojiwa katika swala lolote , adai tatizo ni mfumo na swala la ardhi liko chini ya wizara ya ardhi na si wizara ya ardhi.

Na swala la mifugo na majosho ni swala la halmashauri na si wizara ya mifugo yeye anaonewa tu.

Asema hajawahi kupewa fedha za bajeti kama anavyoomba ajilinganisha na Yesu kuwa anasurubiwa lakini hana hatia.

Updates;

Waziri mkuu anaongea kwa kujumuhisha kwa mawaziri waliosalia na anaanza kwa kauli zake za kuzunguuuka na kuomba radhi kwa waliotendwa na operation tokomeza.

Anachojaribu kusema kama serikali wanatafakari na watafanyia kazi kama serikali kwani operationi ilikuwa chini ya wizara tatu.

Na anaendelea kutazama na kuangalia na anapendekeza iundwe tume ya kuthibitisha hayo kama alivyoshauri Mwanasheria mkuu wa serikali.

Chanzo: Jamii FORUMS

No comments:

Post a Comment