Monday, November 04, 2013

Barrack Obama: Mimi ni Hodari kwa Kuuwa Watu

Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amejisema kuwa yeye ni "hodari sana kwa kuuwa watu," hii ni kwa mujibu wa kitabu kipya kinachohusu kampeni za Urais wa mwaka 2012 kinachoitwa Double Down: Game Change 2012, ambacho kinategemea kutoka siku ya Jumanne (Kesho),.

Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho, Obama, ambaye alishinda Nobel Peace Prize mnamo mwaka 2009, amekumbana na pingamizo kubwa kwa mbinu zake za kutumia ndege zisizokuwa na rubani kwa ajili kukabiliana na magaidi, mbinu ambazo amekuwa akizitumia ikushambulia nchi za Pakistan na Yemen.

Gazeti la Washington Post limeeleza, wakati Obama alipokuwa akizungumza juu ya mipango ya matumizi ya ndege zisizo na rubani ndipo aliposema kwamba yeye ni "hodari sana wa kuuwa watu."

Licha ya hivyo, mshauri wa Obama Dan Pfeiffer alisema kwamba "Rais huchukizwa na uvujaji wa mambo. Sijaongea naye kuhusu kitabu hiki. Sijakisoma. Hata yeye hajakisoma. Ila hapendi kuvuja kwa mambo."

Mamlaka moja ya Uchunguzi iliyopo London imekadiria kwamba Obama aliidhinisha kufanyika kwa mashambulio 326 kwa kutumia ndege hizo.

Toka mwaka 2004, ndege hizo za CIA uzimeuwa watu kati ya 2,500 mpaka 3,600 wakiwemo watu 950 wasio na hatia.


Rais Obama, ambaye alishinda Nobel Peace Prize mnamo mwaka 2009, inakadiliwa kuwa aliagiza kufanyika kwa zaidi ya mashambulizi 325 kwa watu waliodhaniwa kuwa ni magaidi na waaasi.


Obama alipewa Tuzo ya Amani mwaka 2009, katika kipindi ambacho alikuwa hajafikisha mwaka toka achaguliwe kuwa Rais, na alipewa tuzo hiyo kutokana na dhamira yake yakupinga matumizi ya nyukilia.


Mashambulizi ya mauwaji yanayofanywa na ndege za MQ-1 Predator pamoja na nyingine zisizoendeshwa na watu yamekuwa yakiongezeka hasa katika kipindi cha utawala wa Obama, na yeye amekuwa akisimamia na kutetea matumizi ya mbinu hizo.

No comments:

Post a Comment