Thursday, August 15, 2013

Sitatokea Hadharani Mpaka Nirudi Kwenye Umbo Langu - Kim Kardashian (PICHA)

Kim Kardashian
Kesho itakuwa ni mwezi wa pili toka Kim Kardashian alipojifungua mtoto wake wa kike aliyepewa jina la North West, na hakika mvuto wa kipindi ambacho huwa anashiriki kwenye TV umekuwa ni mdogo kutokana na kutokuwepo kwake toka alipojifungua na kuitwa mama.

Hii ni kutokana na yeye kukataa kuonekana kwenye jamii mpaka pale atakaporejea kwenye umbo lake la awali, chanzo kimoja kimeieleza US Weekly, hakuna sababu ya msingi iliyoelezwa kwa yeye kujificha nyumbani kwa mama yake maeneo ya Calif, “moja kwa moja ni ile hali anayoiona juu ya umbo lake.”

Kim hakuweza kuhudhulia kwenye shughuli ya dada yake mdogo Kylie iliyofanyika Nobu Malibu mnamo Aug. 10, huku akielezea kuwa alishindwa kupata gari la kumbebea North kama ndiyo sababu iliyomfanya ashindwe kuhudhulia.

Kim “alisema akija toka nje na kupigwa picha kwa mara ya kwanza anahitaji kuonekana mwenye mvuto, mkali na moto,” chanzo toka ndani ya familia kililieleza jarida hilo, huku kikiongeza kwamba lengo ni kushuka na kufikisha uzito wa paundi 115.

Mpaka sasa Kim ameshakata uzito wa paundi 30 chanzo hicho kilisema, kazi kubwa imekuwa ni katika kuzimalizia nyingine 30.

Kim Alipokuwa Mjamzito

No comments:

Post a Comment