Friday, May 03, 2013

Marapa Kumi Na Moja Waliokufa Wakiwa Na Umri Mdogo

1. Chris Kelly:
Kris Kelly a.k.a Mac Daddy
Kama ilivvyo kwa marapa wengi kabla yake, mmoja kati ya nyota wa kundi la Kris Kross aitwae Chris 'Mac Daddy' Kelly amefariki akiwa na miaka 34 tu. Baada ya kukutwa hajitambui nyumbani kwake Atlanta na kwenda kufia hospitali.

2. Nate Dogg:
Nate Dogg
Nate Dogg jina lake kamili Nathaniel Dwayne Hale - alijulikana sana kuwa mmoja wa wakali wa kollabo, mnamo mwaka 1994 alishirikishwa na rappa mwingine aitwaye Warren G kwenye wimbo wa Regulate, ngoma ambayo ni soundtrack ya muvi ya Above The Rim, muvi ya mchezo wa kikapu ambayo Tupac alishiriki.

Rappa huyo alipata stroke mnamo mwezi December 19 2007 ambayo ilimfanya aparalaizi sehemu ya kushoto ya mwili wake.

Alipata stroke ya pili mnamo mwezi September 2008 na kufa kwa mkanganyiko wa stroke mwezi March 2011.

3. Eazy E:
Easy E
Alijulikana zaidi kama The Godfather wa Gangsta Rap, ni Eazy-E. Jina lake kamili ni Eric Lynn Wright, alikuwa ni mmoja kati ya nembo ya kundi la N.W.A.

4. Big Pun:
Big Pun
Rappa kutoka Puerto Rica maarufu kama Big Pun, jina lake halisi ni Chrisopher Rios. Alianza kujulikana alipofanya kazi na Beatnuts.

Kisha akaanza kufanya kazi kama solo artist na kutoka na kitu cha I'm Not A Player, ngoma ambayo ilikuwa ni kubwa sana ndani ya mwaka 1997 na kumfanya kuwa msanii wa kwanza miondoko ya hip hop kutoka Latino kufika kwenye mauzo ya platinum.

Mafanikio zaidi ya nyota huyo yalishaanza huonekana, ila alikuja kufa gafla baada ya kupata mshtuko wa moyo mnamo mwezi February 2000, alifariki akiwa na umri wa miaka 29 tu.

5. Left Eye:
Left Eye
Lisa, kwa jina la kwenye steji akijulikana zaidi kama Left Eye, alikuwa ni sehemu ya kundi kubwa ndana ya Marekani liitwalo TLC.

Wasichana hao walikuwa na na ngoma kadhaa zilizotamba kama No Scrubs, Waterfalls na Creep, zilizouza zaidi ya rekodi millioni 65.

Ndoto za maisha yake ya baadae zilikatika gafla mara baada kupata ajali ya gari baada ya kushindwa kulimiliki gari vizuri, kipindi ambacho alikuwa anakula sikukuu ndani ya Honduras mnamo mwezi April 2002.

6. Dj La Rock:
Dj La Rock
Rappa wa kwanza kujulikana na kisha kufariki mapema ni DJ La Rock, aliyekuwa anaunda kundi la hip hop la Boogie Down Productions lililokuwa na mkali kama KRS-One.

7. Ol' Dirty Bastard:
Ol' Dirty Bastard
Ol' Dirty Bastard - jina lake halisi ni Russell Tyrone Jones, alikuwa ni memba wa kundi hip hop lililojulikana kama The Wu-Tang Clan sambamba na marappa kama RZA, Method Man na Ghostface Killah. 

8. Guru:
Akijulikana zaidi kwenye steji kwa jina la Guru, huku jina alilopewa na wazazi wake ni Keith Edward Elam, alikuwa ni mmoja kati ya ma-mc wa kimarekani na memba wa kundi la Gang Starr lililoundwa na wana hip hop wawili.

9. Notorious B.I.G:
Akiwa na umri wa miaka 24 jamaa alifariki, Biggie ambaye jina lake halisi ni Christopher George Latore Wallace - alipigwa risasi alipokuwa anaendesha gari kurudi nyumbani kwake Los Angles akiwa anatoka kwenye party mwezi March 1997.

10. MC Proof:
Mc Proof
Mmoja kati ya marafiki wa karibu wa rappa Eminem, msanii kutoka Detroit, MC Proof - jina lake kamili DeShaun Dupree Holton - alikuwa ni mmoja kati ya walioliunda kundi la D12.

11. Tupac
Tupac
Alipigwa risasi na kufa akiwa njiani jijini Las Vegas, baada ya kutoka kuangalia pambano la ngumi kati ya Mike Tyson na Bruce Seldon.

Hakuna aliyekuja kukamatwa baada ya tukio hilo, ila mchunguzi mmoja wa masuala ya habari aitwaye Chuck Philips, aliamua kuendelea mbele zaidi kwenye kesi hii, na kuja na ushahidi uliomuonyesha kwamba memba mmoja wa kundi la LA Southside Crips, ndiye aliyehusika kumpiga risasi Pac, na hii ni ilitokana na mambo ya kulipiziana visasi.

No comments:

Post a Comment