Monday, May 06, 2013

Bomu Arusha: Raia Wa Saudia Wanne Wakatwa




Jeshi la Polisi nchini, linawashikilia watu wa nane kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.

Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.

Miongoni mwa waliokamatwa mpaka sasa ni wageni toka nje ya nchi ambao jeshi hilo limebainisha kama watalii.

Kumatatwa huko kunafuatia mlipuko uliotokea kanisani jijini Arusha jana, ambapo mpaka sasa watu wawili  wanaripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 60 wakiwa wamejeruhiwa.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amelaani tukio hilo na kuliita "kitendo cha kigaidi ".

No comments:

Post a Comment