Arsene Wenger |
Mpendwa Arsene Wenger
Nilikuja kuwa shabiki wa Arsenal mwaka mmoja baada ya wewe kujiunga na klabu, ukaleta mabadiliko makubwa na kutupa sifa ya kuwa na timu nzuri. Ni miaka saba sasa toka tuliposhinda taji letu la mwisho huku timu ikiwa inakwenda kwa kujikongoja.
Swali langu pekee, “Yuko wapi yule Arsene Wenger wa zamani tuliyekuwa tunamfahamu” ambaye alitutoa kwenye aibu mpaka kwenye ufahari, yule aliyeyetuongoza mpaka kwenye mafanikio.
Mechi kila baada ya mechi tunaonekana wabaya zaidi, mipango ya kikosi chako inazidi kuwa mibaya siku hadi siku, unawapa nafasi wachezaji ambao sitawataja nafasi ya kucheza, wakati tukiwaangalia ni wachezaji wanaoonekana kutokuwa tayari kuleta kile tunachotarajia. Unaacha wachezaji kwenye benchi ambao unawaona wakipewa nafasi wanacheza kwa mapenzi toka moyoni mwao. Je ndio kusema umepoteza muelekeo wako ama? Kwa nini unataka kuuvunja uaminifu ambao tulikupa kwa misimu yote ambayo tumekuwa na wewe?
Mara zote umekuwa ukiwauza wachezaji wetu muhimu na kuwabadilisha na wengineo ambao hawawezi kufika karibu ya viwango vyao, na kuacha kuwauza wachezaji ambao mara zote hutuiangusha timu. Tunapoteza imani na timu yetu, kama unachopigania wewe ni kuingia kwenye nne bora hapo sijui ni kitu gani tutakachosema tumefanikiwa? Kama kweli unaijali timu yetu fanya kitu kimoja haraka iwezekanavyo.
Mwisho, mara zote huwa unalalamika juu ya bajeti, wakati sisi sote tunaona unavyouza wachezaji ambao wana thamani sana, na unashindwa kununua wachezaji wanaolingana na hela unazozipata kwa kuuza wachezaji wetu japo hata kwa ukaribu. Tafadhali nakuomba, na tena nakuomba irudishe Arsenal yetu ya zamani.
Hayo ni ambayo naweza kukwambia. Wewe ndiye pekee unayeweza kufuta machozi yetu yanapokuwa yanatoka kwenye macho.
No comments:
Post a Comment