Tuesday, April 23, 2013

Mario Gotze Kuweka Historia Ya Dau Kubwa La Uamisho Bundesliga

Mario Gotze
Mario Gotze anajiandaa kuweka historia ya kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi miongoni mwa wachezaji wote waliowahi kutokea kwenye historia ya Ujerumani, hii ni mara baada ya mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich kutangaza kwamba kiungo huyo wa Borussia Dortmund atajiunga nao kwenye msimu wa majira ya joto.
Bayern wamesema, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atahamia kwenye klabu hiyo mnamo tarehe 1 July baada ya mchezaji huyo wa Kijerumani kuwaelezwa Dortmund nia yake ya kutaka kuondoka.
Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp alisema: "Mario anajua kwa kiasi kikubwa klabu inamuhitaji, ila najua naye anarudisha mengi kwetu pia."
Kiasi cha Euro 37m ambacho ni sawa na Paundi 31.5m kinaaminika kimetumika kumng’oa mchezaji huyo.
Mchezaji wa Kijerumani aliyekuwa anashikiria na rekodi ya juu kwa uamisho ni mshambuliaji wa Mario Gomez ambaye uamisho wake uligharimu kiasi cha Paundi 26.5m kuhamia Bayern toka klabu ya Stuttgart mnamo mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment