Kiungo wa klabu ya Barcelona Cesc Fabregas ilibidi aombe radhi kutokana na kitendo cha timu yake ya Barcelona cha kuifunga klabu ya Manchester City pale alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye tuzo za Brit.
Hii ilikuwa ni masaa 24 mara baada ya ushindi wa magoli 2-0 walioupata kwenye uwanja wa Etihad, Muhispania huyo aliambatana na jaji wa zamani wa X-Factor, Nicole Scherzinger kwenye ukumbi wa O2 Arena kwa ajili ya kwenda kuwatangaza Daft Punk kama washindi wa tuzo ya Best International Group.
Kulikuwa na zomea ya chini chini katika muda ambao alikuwa anapanda kwenye steji na moja kwa moja Fabregas alisema: 'Samahani juu ya usiku wa jana, nimekuja kwa amani.'
Wachezaji wenzake wote wa Barcelona mapema Jumatano asubuhi walirudi kwao Hispaniai ila Fabregas alikwenda London kwa ajili ya shughuli hiyo.
No comments:
Post a Comment