Dingi mmoja mwenye hasira, Deji Kamoru, hivi sasa yupo kwenye mtatizo makubwa kutokana na kitendo chake cha kumrusha mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 14, Aishat toka gorofa ya tatu mara baada ya kumfuma akiwa na mpenzi wake kwenye chumba chake cha kulala.
Imeelezwa, mwanzoni aliifunga kwa kamba mikono ya Aishat, kumtesa na mwisho kumtupa toka kwenye gorofa ya tatu nyumbani kwao Mtaa wa Oroyinyin, Kisiwa cha Lagos, Jimbo la Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria.
Vyanzo viligundua kwamba wakati Aishat alipotua chini, aligonga kichwa chake kwenye kitu chenye ncha kisha akapoteza fahamu.
Binti huyo alikimbizwa Hospitali ya Lagos Island General iliyopo jijini Lagos ambapo kwa sasa yupo chumba cha watu mahututi.
No comments:
Post a Comment