Monday, December 09, 2013

Mshabiki wa Manchester United Nchini Kenya Ajiua kwa Kujirusha Toka Gorofani Baada ya Kipigo cha Newcastle [VIDEO]


Jamaa mmoja anayeaminika kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United mnamo siku ya Jumamosi usiku kwenye Jimbo la Pipeline jijini Nairobi, hii ni mara baada ya timu yake kufungwa goli 1-0 na Newcastle.

Polisi wamesema John Jimmy Macharia, mwenye miaka 23, alijirusha toka kwenye gorofa ya saba mara baada ya timu yake kupoteza mchezo mwengine kwenye mechi iliyochezwa Jumamosi jioni.
 

Shuka chini kutazama video ya tukio hili...

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake kuwa hawezi kuona timu yake ikifungwa mfululizo kabla ya kuamua kujirusha na kufa papo hapo.

“Wote walioshuhudia wanasema sababu ya jamaa kujiua ni kutokana na timu yake kufungwa ila maafisa wanaendelea kuongea na watu waliyekuwa nae kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.


Kibue aliwashauri vijana wa jiji hilo kutambua kwamba Ligi Kuu ya Uingereza ni kama aina nyingine ya michezo hivyo wanapaswa wasiwe wanaguswa sana kihisia na michuano hiyo.

“Sio mara ya kwanza kumpoteza kijana sababu ya Ligi ya Uingereza, ambayo ipo mbali na sisi, wanahitaji kujua kwamba hii ni michezo tu,” alisema Kibue.

Mwili wa marehemu ulitolewa na kupelekwa mochwari na polisi waliofika pale. Macharia inasemekana aliangukia kichwa pindi alipojirusha toka kwenye gorofa hilo.

Angalia video hapo chini...
 
 

No comments:

Post a Comment