Dola Indidis |
Serikali ya nchi ya Israel imefikishwa mahakamani na Wakili
mmoja wa Kenya kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, International Criminal
Court of Justice (ICJ), kwa kosa la kumtesa na kumuuwa Yesu Kristo, kitendo
ambacho Wakili huyo anadai kilikuwa ni kinyume na sheria, kwa mujibu wa taarifa
ya vyombo vya habari.
Wakili huyo wa Kenya aitwaye Dola Indidis anadai Waisrael na Wayahudi
wanahusika moja kwa moja na kuhusika na kifo cha Yesu Kristo na inatakiwa
washtakiwe kisheria, hii ni kwa mujibu wa Jerusalem Post.
Indidis, ambaye ameipeleka kesi hiyo ICJ ndaini ya The
Hague, pia anawashitaki Tiberius, kiongozi
wa Rome wa mwaka 42 BCE, “Pontius Pilate, baadhi ya viongozi wa Kiyahudi,
Mfalme Herod, Serikali ya Italia, na Serikali ya Israel,” kwa mujibu wa Gazeti
hilo.
Indidis anatumia Biblia kama ushahidi wake wa kwanza kwenye
kesi hiyo.
“Ushahidi kwa sasa upo kwenye kumbukumbu za Biblia, na
huwezi kuipinga Biblia,” Indidis alinukuliwa akisema kupitia taarifa ya
habari ya Citizen.
Indidis pia akasisitiza “Serikali ya Israel
ambayo ipo madarakani ndiye mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi
hiyo,” taarifa hiyo ilisema.
Duh! Kali ya mwaka..ngoja tuone!
ReplyDelete