Sunday, May 05, 2013

Taarifa Na Picha Za Matukio Kwenye Mlipuko Wa Kanisa Arusha

Kanisa La Olasiti
Kanisa Katoliki la Parokia ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linategemea kupandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na kile kinachesemekana kuwa ni bomu na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa mashuhuda mbalimbali jumla ya watu watatu inasemekana wamefariki mpaka sasa, huku taarifa ya Jeshi la Polisi nchini ikisema ni mtu mmoja tu aambae amethibitishwa kufa kutokana na tukio hilo.

Shuhuda mmoja amesema watu watatu wamefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya sana, baadhi wakiwa wamekatika viungo vya miili yao.

Nilipoongea na shuhuda mwengine aitwaye Tinah Kivuyo yeye alisimulia juu tukio hilo alivyoliona, "wakati watu wanaingia kwenye ibada huku kukiwa na mkusanyiko mkubwa wa waumini, ghafla bomu lililipuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja pale pale na wengine wengi wakiwa ni majeruhi"

Aliendelea kwa kusema "damu zilitapakaa ikiashiria kuwa watu wengi wamejeruhiwa vibaya na bomu hilo huku hali zao zikiwa si nzuri, baadhi ya majeruhi wamekimbizwa kwenye hospitali za Mount Meru, Seriani na St Elizabeth."
Inasemekana bomu hilo lilirushwa na mtu asiyejulikana, huku watu wengi wakihusisha tukio hilo na chuki za kidini zinazoendelea kupandikizwa kwa kasi.
Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini kwa kuhusika tukio hilo.
Polisi Kwenye Eneo La Tukio

Kanisa Kwa muonekano Wa Mbali

Waumini Na Wanachi Wakiwa Eneo La Tukio
Habari zaidi zitafuata......

No comments:

Post a Comment