Sheikh Ponda Akiongea Na Waandishi Alisema "Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." |
Hii ni kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili, Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo hicho kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia ya kutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyokwenye mahakama hiyo paliibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo, pia alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa
No comments:
Post a Comment