Sunday, May 12, 2013

Gari Latumbukia Kwenye Mtalo (AJALI)

Ajali iliyohusisha magari mawili imetokea mchana wa leo maeneo ya Tabata Segerea karibu na Lake Oil (Kwa msangi).

Ajali hiyo ilitokea pale ambapo gari moja ilipojaribu ku-over take ili iweze kuingia kituo cha mafuta.

Dereva alishindwa kumiliki usukani na ndipo alipogongana na gari lingine lenye namba za usajili T 462 CCD aina ya Nissan, gari ambalo limeharibika vibaya baada ya kutumbukia kwenye mtalo, pia gari lingine ni lenye namba za usajili T 283 CEN aina ya Mitsubishi na limeharibika kiasi.

Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyeumia.

Powered By David P. Mayunga (Peace Mayda)

No comments:

Post a Comment