Sunday, May 19, 2013

Busta Rhymes Kufanya Kazi Na Nick Pamoja Na Drake

Mwanamuziki wa miondoko ya hip hop toka nchini Marekani Busta Rhymes, ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Cash Money Records, ila kiukweli rapa huyo hajawahi kufanya kolabo na nyota wawili wa lebo hiyo.

Alielezea kwenye jarida la Rolling Stone kwa nini mpaka sasa hajawahi kuingia studio kurekodi na Nicki Minaj au Drake.


"Um . . . na hujawahi kusikia kitu chochote kati yangu na Nicki. “Remix ya Roman’s Revenge,”  kile kilikuwa ni kitu ambacho nilikifanya kivyangu. Haikuwa remix rasmi, kwa hiyo kiufundi sijawahi kuingia naye studio".

"Kwa hiyo Drake na Nicki, hatujawahi kufanya kazi, hapana.... mara zote huwa inatokea wakati muda unapokuwa ni muafaka. … tuliongea mwanzo".

"Niliwahi kufanya mazungumzo mara kadhaa na Drake ya kutengeneza rekodi moja, tumewahi kuwa studio tukijaribu kufanya kitu studio. Sawa pia na Nicki. Ni kwamba tu . . . tunapoanzisha wazo, wakati mwingine kunatokea mkanganyiko, ni majukumu tu...."

Mwaka 2012, Busta Rhymes aliachia album yake ya tisa iliyoitwa, Year of the Dragon.

No comments:

Post a Comment