Tuesday, May 28, 2013

Amanda Bynes Amshambulia Rihanna kwa Tweets za Kashfa

Mwanzoni Walikuwa Marafiki
AMANDA Bynes amemshambulia Rihanna mara baada muigizaji huyo wa Marekani kuandika maneno ya kashfa kwa Rihanna kupitia Twitter.

Rihanna mwenye umri wa miaka 25 alionekana kukasirishwa baada ya kukuta Tweet toka kwa Amanda iliyoandika “Rihanna ni mbaya anapojaribu kuwa mweupe”.

Huku ikiendelea kwa kusomeka inawezekana  muonekano wake ndio uliosababisha jamaa yake wa zamani Chris Brown amtukane akiandika: "Chris Brown alikupiga sababu wewe sio mzuri wa kutosha."

Amanda ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa muimbaji huyo wa  Barbadian RiRi, alizifuta tweets zake muda mchache mara baada ya kuzituma, kipindi ambacho tayari Rihanna alishaziona na kurudisha maneno yaliyosema: “Angalia nini huja kutokea pale wanapositisha kujihusisha?” akijaribu kukumbushia kipindi kimoja cha TV nchini Marekani ambacho vijana wenye matatizo husaidiwa katika kuwawekwa sawa pale ambapo wanaonekana kuwa wamepotea.

Soma chini Tweets za Amanda kwa Rihanna:

No comments:

Post a Comment