Tuesday, April 16, 2013

SHINDANO LA WAJAWAZITO KWA KIVAZI CHA BIKINI

Jumla ya wajawazito arobaini wa ujauzito wa miezi zaidi ya mitano walijitokeza kushiriki kwenye shindano la wajawazito katika kivazi cha bikini. Shindano hilo ambalo limefanyika nchini Marekani pande za Houston, limeshuhudia mwanadada Jennifer Clay akiibuka mshindi katika kipindi ambacho ujauzito wake ukiwa na wiki thelathini na mbili. Huu ni mwaka wa nane toka kuanzishwa kwa shindano hilo ambalo huandaliwa na kituo kimoja cha Radio kupitia moja kati ya vipindi vyake, limekuwa likipigwa na jumuia, taasisi na watu mbalimbali. Dunia ndio hii na haya ni baadhi ya mambo yake...! Ninyi si ni mabingwa wa kuiga kila kitu..? Basi igeni na hili..! Una lolote la KUCHANGIA..?

No comments:

Post a Comment