Tuesday, April 16, 2013
REEBOK WAVUNJA MKATABA WAKE NA RICK ROSS
Hatimae yametimia, kampuni ya vifaa vya michezo ya Reebok imesitisha mkataba wake na Rick Ross. Sababu kuu ni wimbo wa msanii huyo uitwao U.O.E.N.O ambao mashairi yake yanachochea na kuhalalisha suala la ubakaji.
Makundi ya kupinga ubakaji na yale ya wanawake walianzisha kampeni ya kuitaka kampuni ya Reebok kuvunja mkataba na Ross.
Licha ya kuomba msamaha leo hii Reebok wametoa tamko la kusitisha mkataba wao na bosi huyo wa May Batch Music.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment