Tuesday, April 16, 2013
KWA DADA ZANGU: UTAJUAJE KAMA ANAKUPENDA
Je wewe ni mmoja kati ya wanawake ambao upo na mwanaume karibu na huyo mwanaume hutumia muda mwingi na wewe ila hujui kama ana hisia au yupo kiurafiki tu?
Hizi hapa ni njia chache zakufahamu kwamba huyo mtu anahitaji kuwa zaidi ya rafiki:
1. Hukupigia Simu Bila Sababu
Kama mwanaume anakupenda, atakupigia simu mara kwa mara, japo kukusalimu na kujua siku yako inakwendaje. Atatafuta kila njia ili aweze kufanya mawasiliano na wewe hata mazingira yawe magumu kiasi gani kwake.
2. Atahitaji Kuwa Karibu Na Wewe
Kama mwanaume anakupenda, atafanya kila jitihada kukuona mara kwa mara. Kama kiukweli anakupenda, atahitaji kutumia muda wake mwingi kuwa na wewe, haijalishi katika muda huo ni kitu gani mtakuwa mnafanya pamoja, cha msingi kwake ni kutaka kuwa na wewe. Mwanaume ambae hafurahii kampani yako hakika wewe si wa moyoni kwake.
3. Katika Maisha Yake Huwa Na Muda Kwa Ajili Yako
Licha ya ratiba zinazotoka na majukumu tuliyonayo katika maisha ya Dunia ya sasa, kama mwanaume anakupenda lazima atakuuwa muda kwa ajili yako. Hata kama atakupigia simu na kukueleza kama anataka kusafiri kwa kwa siku kadhaa ni lazma ataomba kukuona kabla hajasafiri, atapenda kuongea na wewe kabla hajasafiri, au kukueleza mipango yake pale atakaporudi.Yote hayo ni katika kukuonyesha kwamba yeye ni muaminifu juu yako.
4. Rafiki Zake Watakufahamu
Kama huyo mwanaume kiukweli anataka kuwa na wewe, atakutambulisha kwa rafiki zake wa kiume. Marafiki wa mwanaume ni watu wanaomuunga mkono, pia atakutambulisha kwa ndugu zake wa pembeni nje ya wale wa damu moja. Kama mwanaume huwaambia rafiki zake kuhusu wewe na kukutambulisha kwao na kukufanya wewe sehemu ya maisha yake, basi hakika atakuwa na na hisia za kweli na wewe.
5. Atakusikiliza
Dalili nyingine ya kuiangalia ni vile ambavyo atakuwa anakusikiliza na kuitikia kile unachomuambia. Mwanaume anayejali kuhusu wewe atahitaji kujua nini unataka kusema na jinsi gani unajisikia kuhusiana na vitu flani. Mwanaume akiwa anakupenda kweli, si tu kwamba atakufanya kuwa sehemu ya mazungumzo yake, ila atakuuliza juu ya mawazo yako, kukusikiliza kwa makini, na kuitikia na kutekeleza kwa dhati kile unachomwambia.
MSISITIZO: Njia muhimu ya kufahamu kama mwanaume anakupenda ni kuangalia kwa makini matendo yake. Wanaume tofauti na walivyo wanawake, siku zote ni wazuri sana kwa maneno, ila mwanaume anayekupenda atakuonyesha anachoongea kwa namna yoyote ile.
Fungua macho yako na kuwa makini ili usilikose penzi la ukweli.
Je wa kwako anafanya haya...?
NAAMINI NIMESAIDIA KUTOA MWANGA JAPO KWA KIASI FULANI. HEBU JARIBU KUFANYIA KAZI KISHA UNIPE MATOKEO.
Dan Chibo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment