Tuesday, April 16, 2013

HEBU SIKIA HII STORI

Kuna wanawake wawili magari yao yaligongana, mmoja ana gari aina ya Vitz na mwengine Land Cruiser VX. Kila mmoja akashuka kwenye gari lake na kwa hasira wakaanza kutoleana maneno ya kashfa. Mwenye VX alimtukana sana mwenye Vitz ambae ndiye alikuwa na kosa. Mwanamke mwenye gari aina ya Vitz akaamua kumpigia simu mumewe "Mume wangu nina tatizo nimegonga gari ya mtu" Mume: Jamani niko kwenye mkutano hebu litatue mwenyewe." Yule mwenye VX nae akampigia simu Boyfriend wake "Darling kuna mjinga kagonga gari uliloninunulia please njoo." Haijapita muda jamaa akafika.....! Daaah kumbe jamaa ndie Mume wa Mwanamke mwenye gari aina ya Vitz...! Unajua nini kiliendelea..? Hebu fanya kuotea..!

No comments:

Post a Comment