Tuesday, April 16, 2013
DADA ANANIOMBA NIZAE NA MUME WAKE
Mimi na dada yangu ni yatima. Wazazi wetu walifariki wakati nina miaka nane. Dada yangu mkubwa aliolewa miaka 12 iliyopita na hajabahatika kupata mtoto. Baada ya uchunguzi wa muda mrefu, alielezwa kwamba hatokuwa na uwezo tena wa kupata watoto.
Jana usiku, alikuja nyumbani kwangu akiniomba nimbebee mimba kwa kutembea na mumewe. Alisema kwa kuwa sisi ni dada wa damu moja, itakuwa kama mtoto ni wa kwake. Hataki mume wake atoke nje kwenda kwa ajili ya kutafuta mtoto, maana anajua mwisho wa siku inaweza kuja kula kwake kwa yeye kutimuliwa kwenye nyumba. Akasema itakuwa ni sawa sababu kiukweli sina mahusiano na mtu yoyote kwa sasa.
Pia akanieleza kwamba hilo jambo hajamueleza mume wake, sababu alikuwa anasubiri jibu langu kwanza.
Nilichanganyikiwa na sikujua nini cha kumwambia. Nilimuomba anipe muda nifikirie juu ya hilo.
Nahitaji ushauri wenu.
Wadau tunamsaidiaje huyu dada...?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment