Tuesday, April 16, 2013
CHRIS BROWN na RIHANNA : Waachana RASMI
Sasa tunaweza kukifunga rasmi kitabu cha mapenzi ya Rihanna na Chris Brown, kwa mujibu wa chanzo cha karibu, imetangazwa rasmi kwamba mahusiano ya wawili hao yamevunjika rasmi kwa sasa.
Chanzo hicho kimeongeza na kusema, wawili hao wameachana kutokana na kuchoshana na mapenzi ya kukimbizana kila mara. Chanzo hicho pia kimesema, licha ya kwamba Rihanna ataendelea kumpenda Chris Brown ila ameamua bora aendelee na maisha yake na ataendelea kufuatilia biashara zake na kazi zake.
Kwa sasa Rihanna yupo kwenye hatua za mwisho za ziara ya Diamonds, ziara ambayo anategemea kufunya kwenye miji mbalimbali, ambapo kwenye ziara hiyo anategemea kuwa pamoja na watu wake wa karibu, pia hivi karibuni Rihanna anategemea kuzindua pafyumu yake mpya huku akiendelea kujikita zaidi na mambo ya fasheni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment