Tuesday, March 20, 2012

"NICHUMU" Mbioni Kwenye Kideo - Bob Jr.


Sharobaro Bob Jr.
MSANII mwenye staili ya kipekee bongo, Bob Junior, amesema kuwa anatarajia kupelekea videoni ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nichumu’, na baada ya hapo kuipelekea redioni.
Akizungumzia wimbo huo msanii huyo alisema kuwa ngoma hiyo ameimba kuliko zote alizowahi kuzitoa hivyo anaamini mtu akiyeisikiliza mara moja hatochoka kutaka kuisilikiliza tena.
Alisema kuwa hata hivyo kikubwa alichokiimba ndani ya kazi hiyo ni mapenzi ambayo anaamini hayana kikomo na mwisho wa kupenda ni pale mungu atakapokuchukua.
“Hakuna asiyejua raha ya kupendwa hivyo hii ni ngoma ambayo imejaa mapenzi na naamini  mashabiki wangu wataipenda kutokana na ubora wake,” alisema.

Chanzo: DarTalk.

No comments:

Post a Comment