Thursday, February 20, 2014

YAMETIMIA: Atupwa Jela kwa Kuposti Picha za Utupu za Aliyekuwa Demu Wake Kwenye Facebook [PICHA]

Hakika mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake, wengi wetu tumekuwa tukiangalia zaidi upande mmoja wa hili nao si mwengine bali ni wa faida, tukisahau kuangalia upande wa pili ambao ndio wenye athari kubwa zaidi, ni upande ambao watu wengi waliokutana na madhara yake wamefikia hatua ya kujuta na hata kujitoa kabisa kwenye mitandao hii.

Mahakama moja ya Accra, Ghana imempa adhabu ya kwenda jela kwa miezi sita kijana mmoja aliyejtambulika kwa jina la Henry Alibah, mara baada ya kupatikana na hatia ya kuposti picha za utupu za aliyekuwa demu wake mara baada ya msichana huyo kuvunja mahusiano kati yao.

Inaelezwa kwamba mvulna huyo aliposti picha za msichana huyo zikimuonyesha akiwa kama nyota wa filamu za ngono anayelipwa kutokana na kufanya tendo hilo, huku pia kijana huyo akiweka namba ya simu  ya msichana huyo sambamba na picha hizo.

No comments:

Post a Comment