Sunday, February 09, 2014

Liverpool Yaibanjua Arsenal Goli 5-1 Ndani ya Anfield

Liverpool wamecheza moja kati ya mchezo mzuri ndani kwa msimu huu wakifanikiwa kupata ushindi wa goli 5-1 dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Anfield.

Magoli manne ya haraka ndani ya dakika 20 za kipindi cha kwanza yaliiufanya mchezo uwe nyuma ya vijana wa Arsene Wenger.

Martin Skrtel alifunga mara mbili ndani ya dakika 10 na kuwafanya Liverpool wawe kwenye moto, kisha baadae Raheem Sterling na Daniel Sturridge waliipa timu ya nyumbani magoli mawili ya zaidi yaliyopelekea ubao kusomeka 4-0 kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.

Liverpool walifanikiwa kuongeza goli la tano lililofungwa tena na Raheem Sterling huku goli la Arsenal likifungwa na Mikael Arteta kwa mkwaju wa penati kwenye kipindi cha pili.

Cheki hapo chini picha zaidi....













No comments:

Post a Comment