Friday, February 14, 2014

17 au 41: Lazio Yamtetea Mchezaji Wake Baada ya Kuonekana Kuwa Amedanganya Umri Wake [PICHA]

Moja kati ya klabu kubwa ya Italia, Lazio, wamejitokeza rasmi na kumtetea mchezaji wao wa kiungo mwenye umri wa miaka 17, Joseph Minala, kuhusu umri wake ya kuwa sio miaka 41 kama ambavyo imekuwa ikizungumzwa.

Mapema wiki hii Minala alizua gumzo kubwa kutokana na muonekano wake mara baada ya kuwa mmoja kati ya wachezaji wadogo waliopandishwa kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Lazio.

Amekuwa akishambuliwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakisema kuwa amedanganya umri wake, ikionekana kuwa ana umri zaidi ya miaka 17.

Minala alipokea maswali mengi mara baada ya kuposti picha ya hapo chini  kupitia Instagram:

No comments:

Post a Comment