Tuesday, August 13, 2013

Hatimaye Queen Latifah Azungumzia Juu ya Ishu Inayomuandama ya Usagaji (PICHA)

Queen Latifah Akiwa na Janette Jenkins
Mara zote amekuwa ni mtu wa kutopenda kuzungumzia maisha yake ya ndani, kitu ambacho kimekuwa ni mjadala mkubwa miongoni mwa mijadala inayomuhusu yeye.

“Sidhani kama inahitajika kujadili juu ya maisha yangu binafsi kwenye show hii au hata show nyingine,” alisema Latifah alipokuwa akiongea huku akiwa anapata mlo wa mchana.

“Kuna sehemu ya maisha yangu ambayo jamii na mimi tunashirikiana, ila kuna maisha ya sehemu nyingine ambayo ni yangu pekee ambayo inabidi yawe yangu, kivyangu vyangu.” alisema Queen Latifa.

“Ni jukumu lake kuchagua kipi ambacho angependa kuongea,” alisema Holly Jacobs, muongozaji mkuu wa vipindi vya Sony Pictures Television. “Haiwezekani kuwa sawa, kwangu mimi sababu tunafanya kipindi kikubwa, kipindi cha uburudishaji na kufurahia maisha yote.

Kuna tofauti kati ya kuzungumzia maisha binafsi ya mtu na mtazamo wa mtu pamoja na upokeaji wa wanadamu kwa vile wanavyoliona jambo au kulitafsiri.

Na naheshimu kwamba watu wanahitaji kuweka mipaka kwa chochote wanachohitaji kukizungumzia.”

Wamiliki 10 Matajiri wa Vilabu vya Soka Duniani, Sheikh Mansour wa Man City Hayumo


10. Roman Abramovic (Chelsea, England) $10.2 billions

9. John Fredricksen (Velerenga, Norway) $11.5 billions

8. Paul Allen (Seatle Sounders, United States) $15.0 billions.

7. Francois Pinault (Stade Rennes, France) $15.0 billions.

6. Rinat Akhmetov (Shakhtar Donetsk, Ukraine) $15.4 billions.

5. Lakshmi Mittal (Queens Park Rangers, England) $16.5 billions.

4. Alisher Usmanov (Arsenal, England) $17.6 billions.

3. George Soros (Manchester United, England) $19.2 billions.

2. Amancio Ortega (Deportivo La Coruna, Spain) $57 billions.

1. Carlos Slim (Club Pachuca, Mexico, Club Leon, Mexico, Real Oviedo, Spain) $73.0 billions.

DOKEZO: Sheikh Mansour, mmiliki wa timu ya Manchester City na Nasser Al-Khelaifi, mmiliki wa PSG wameachwa kwenye horodha hii sababu utajiri wao ni wa kifamilia na hapa wa waliokuwa wanaangaliwa ni wale wenye utajiri binafsi....

CHANZO: Sulia.com

Bilionea Msuya Kuzikwa Leo, Jeneza Lafunguliwa kwa ‘Rimoti’

Marehemu Erasto Msuya
Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’

Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya ‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, zaidi ya Sh100 milioni zimepangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.

"zaidi ya Sh100 milioni zimepangwa
kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi"
  
Imesema
Kamati ya Mazishi

CHANZO: Gazeti Mwananchi

Pafyumu ya Beyonce Yatajwa Kuwa Bora Kati ya Pafyumu za Watu Mashuhuri Duniani


Pafyumu ya mwanamuziki maarufu toka nchini Marekani Beyonce Knowles iitwayo Heat (Catch The Fever) imetajwa kuwa ndiyo pafyumu bora kimauzo miongoni mwa pafyumu za watu mashuhuri Duniani kwa sasa.

Je Umeshawahi Kumuona Cheetah Akicheza Mpira wa Miguu...? Huyu Hapa... (PICHA)

Aina hizi za Cheetah wanaocheza mpira wa miguu huwa hawana haja ya kufata sheria rasmi za mchezo huo. Wageni kwenye Lodge ya Akwaaba iliyoyo Rustenburg, Afrika Kusini hufanikiwa kuona vipaji vya paka hawa wakubwa kwenye sehemu ya wazi ya eneo hilo.

Cheetah hawa ambao ni kaka na dada wanaojulikana kwa majina ya Lucky na Leila wameishi na kukuzwa na binadamu toka walipokuwa wadogo mpaka sasa wakiwa na uwezo wa kukimbia kilometa 70 kwa saa.

Wanyama hawa wenye umri wa miaka minne sasa mbali ya uwezo wa kukimbia kwa kasi pia wana uwezo wa kupokea pasi, kukokota mpira na kutoa pasi.

Chini ni maelezo kwa picha.....

READ MORE:  http://news.naij.com/42286.html







Kutana na Waschana Hawa Walioamua Kutembea Mitaani Wakiwa Wamevaa Jeans na Bra tu.... (PICHA)

Nini ni hasa ambacho kinaweza ingia akilini kwako kutokana na kitendo cha waschana hawa kuamua kutembea mitaani wakiwa wamevaa pea ya jeans, viatu virefu na bra pekee....?

Hakika si kitu kingine bali ni moja kati ya sehemu za promosheni ya aina mpya ya InvisaBra ambayo haina mikanda au kamba za kushikilia (strapless, backless brá) ikifahamika kuwa moja kati ya aina ya bra iliyochota mioyo ya wanawake wengi Duniani kwa sasa.

Wiki iliyopita mitaa ya Regent, jijini London ilikumbwa na kisanga hiki ikishuhudia waschana wapatao kumi hivi wakionekana kupita mitaa hiyo huku wakiwa wamevaa viatu virefu, jeans za blue na bra hizo.

TBC fm TOP 20 Wiki Iliyoishia August 11

1. Pesonally  - P Square
2. Yahaya - Lady JD
3. Kama Huwezi - Rama Dee Feat. Lady JD
4. Majanga - Snura
5. I Love You - Kassim Mganga
6. Bila Kukunja Goti - Mwana FA & AY Feat. J Martin 
7. Nani Kamwaga Pombe Yangu -  Madee Feat. Raymond
8. Antenna - Fuse ODG 
9. Nakupenda Pia -Wyre Feat. Alaine 
10. Joto Hasira -Lady JD Feat. Prof. Jay
11. Nikumbatie - Joh Makini Feat. Fundi Samweli
12. Sina Imani - Shetta Feat. Richie Mavoko
13. Shout Up - Jos Mtambo Feat. Pipi 
14. Wasi Wasi - Vumbe
15. Ukimuona - Diamond
16. Muziki Gani - Ney Wamitego Feat. Diamond
17. Weka Ngoma - Darasa Feat. Ditto
18. My Baby - Quick Racka Feat. Ngwea & Shaa
19. Love Me - Izzo B Feat. Barnaba & Shaa
20. Nakomaa Na Jiji - Shilole {MPYA}

Kila siku ya Jumapili Saa 8 mpaka 10 Jioni kupitia TBC fm na Dan Chibo