Wednesday, December 11, 2013

R.Kelly Afanya Kosa Kubwa Ambalo Hatolisahau


Hivi ndivyo ambavyo hutokea wakati biashara kwa njia ya vyombo vya habari inapokwenda ndivyo sivyo. Mwanamuziki R.Kelly siku za nyuma kidogo alielezea juu ya mpango wake aliouita #AskRKelly ambao alipanga utumike kwenye Twitter kwa ajili ya kipindi cha maswali na majibu (Q & A session) kwa ajili ya kupromoti albam yake mpya.

Toka mpango huo uanze tweets nyingi za ajabu zimekuwa zikiingia na kumshambulia huku nyingi zikiwa zanambeza, kumkashifu na hata kumtukana kwa matusi ya nguoni.

Kwa njia ya Twitter hivi ndivyo alivyouanzisha mpango huo:


Najaribu kufikiri.., Ni nini hasa kilimfanya aone kama hili lilikuwa ni wazo zuri kwa yeye kujiingiza kwenye mambo haya? Nadhani mapema tu alitakiwa afunge ukurasa huo ila afahamu kwamba Dunia huwa haisau aina ya mambo kama hayo.

Ni nini hasa yeye na meneja wake wa mambo ya media walikuwa wakifikiria? Labda inawezekana yeye mwenyewe alijitia kitanzini au ni meneja wake ndio aliopanga huo mchongo. Vyovyote vile ilivyo, atakuwa anajimaliza!


Soma majibu mabaya na yakusikitisha toka kwa mashabiki:













No comments:

Post a Comment