Wednesday, December 25, 2013

Nyota wa Filamu Idris Elba Ajeruhiwa Baada ya Gari Kupinduka Akakitengeneza Filamu


Muigizaji wa filamu wa Kiingereza Idris Elba amenusurika ajali mara baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka alipokuwa akishuti filamu kwa ajili ya makala ya TV.

Nyota huyo wa  filamu ya “Mandela: Long Walk to Freedom” ambaye alikuwa nchini Finland kushuti makala hiyo ya BBC ya “Idris Elba: King of Speed” alijikuta akipinduka na gari hiyo.

Elba alieleza gazeti la The Sun, “Sikuhitaji kufanya vile tena, ni mara ya kwanza kupindua gari. Sikuwa naendesha kwa spidi, gari lilikuwa na fikira zake ilipoenda kugonga kizuizi. Nikakata kona na ndipo tulipopinduka.”

Makala hiyo yenye sehemu mbili inategemea kuonyeshwa ndani ya UK mnamo Dec. 26 na 27.

No comments:

Post a Comment