Wednesday, December 11, 2013

Cristiano Ronaldo Avunja Rekodi Klabu Bingwa ya Ulaya


Nyota wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amekiri kuwa kilikuwa ni kitu "maalum" kwa yeye kuweka rekodi mpya ya ufungaji wa magoli kwenye hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Ronaldo ambaye pia ni kapteni wa timu ya Taifa ya Ureno, jana Jumanne alifanikiwa kufunga goli lake la tisa katika mechi tano alizocheza, kwenye mechi waliyoshinda dhidi ya Copenhagen - mchezo ambao pia mshambuliaji huyu alikosa penati - ila mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameonya kwamba bado hajarudi kwenye kiwango chake mara baada ya kutoka kwenye majeraha.

No comments:

Post a Comment