Kimbunga kikubwa kimeikumba Philippines mnamo siku ya Ijumaa, kikiuwa zaidi ya watu 10,000 na kujeruhi watu wengi huku wengine kutofahamika walipo.
Kimbunga hicho ambacho kimepewa jina la Haiyan, kinaaminika kuwa ndio kimbunga kikubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia Duniani kinakadiliwa kuwa na ukubwa wa 235mph kwa 170mph.
Kimbunga hicho kimeharibu miundombinu mingi, huku kikisababisha huduma za umeme na mawasiliano kuvurugika kitu ambacho kimesababisha usumbufu na uhalibifu mkubwa sana.
Maelfu ya nyumba yameanguka na kubomoka huku miili ya binadamu ikiwa imetapakaa mitaani.
Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea Barani Asia ni kinategemea kufika Pwani ya nchi ya Vietnam siku ya Jumapili asubuhi huku ikielezwa kwamba kuna uwezekanao mkubwa wa idadi ya waathilika kuongezeaka.
Angalia picha za kuhuzunisha zaidi hapo chini:
No comments:
Post a Comment