Monday, July 22, 2013

Je ni Vibaya Kuoa au Kuolewa na Mume au Mke wa Rafiki Aliyefariki? (MUHIMU SOMA BARUA HII)

Mapenzi na Upweke
Hakika kifo ni kitu ambacho kila mmoja wetu ni lazma akipitie, wengine hupoteza maisha kwenye ujana wao na wengine hufariki wakiwa wazeee kabisa.

Katika muda wowote ule ila bado inabaki kuwa vyote ni vifo, iwe leo au kesho ila ukweli unabaki pale pale kwamba siku moja tutakuja kuyaaga haya maisha na kuwaacha wanaotupenda kuwa kwenye majonzi makubwa.

Kwa sasa wewe  ni mzima na unasoma habari hii, ningependa kukuuliza hili swali: unadhani sio sahihi kwa rafiki yako wa karibu kumuoa mkeo au kuolewa na mmeo pale utapofariki?

Wakati unatafakari juu ya swali hili, fanya kujiweka kwenye viatu hivi huku ukisoma barua hii iliyotumwa na mmoja kati ya wadau ambaye alikuwa anataka kupata ushauri na majibu toka kwetu juu ya hali hii:
 

Habari DC,

Nilikuwa na rafiki ambaye namchukulia zaidi ya best friend na tulifahamiana toka tukiwa wadogo.
Alifariki muda ama miaka minne iliyopita na mume wake anahitaji tuingie kwenye uhusiano wa ndani zaidi utakaotufikisha kwenye ndoa.
Yeye na marehemu rafiki yangu ambae alikuwa mke wake  wa ndoa walibahatika kupata watoto wawili na kwa kipindi sasa nimekuwa nikitembelea nyumbani kwake mara kwa mara kuwaona watoto sababu nimetokea kuwapenda.
Kilichopo na kinachoendelea sasa, nafikiri mume wa marehemu rafiki yangu ananiona mimi  kama mama yao hao watoto na anataka tutambulike rasmi kwa ndugu jamaa na marafiki juu ya nia yake ya kunifanya niwe mke wake.
Sijui nini cha kufanya.....
Je ni vibaya kwa mimi kuolewa na yeye...?

No comments:

Post a Comment